NAPE NNAUYE AELEZA ALICHOAMBIWA NA TUNDU LISSU WAKITOKA BUNGENI JANA

Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye ameeleza alichoambiwa na Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu jana Alhamisi mchana wakati wakitoka bungeni huku wakicheka.

Nape amesema Lissu alimwambia, “Wewe Nape ni mjomba wangu, kwa nini unabaki CCM? Mimi na wewe tunafuatiliwa na jamaa zako wakitumia gari moja. Mimi na wewe ni watuhumiwa, hama CCM mjomba.”


Lissu alipigwa risasi jana Alhamisi mchana na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na baadaye usiku alihamishiwa Hospitali ya Aga Khan ya Nairobi nchini Kenya.

Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini jana wakati Lissu akipelekwa Kenya alisema ameambatana na mkewe, madaktari wawili wasio na mipaka; Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.

Ndege iliyomsafirisha iliondoka katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma saa sita na robo usiku.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post