KUTANA NA MTOTO MCHANGA ALIYEOTA MENO SABA MARA TU BAADA YA KUZALIWA

Ni jambo unaloweza kuliita ni ajabu ambapo mtoto wa umri wa mwezi mmoja tangu kuzaliwa kuota meno saba na kusababisha Madaktari kumfanyia upasuaji kuyaondoa meno hayo.

Tukio hilo limetokea India ambapo mmoja wa Madaktari waliomfanyia upasuaji mtoto huyo, Meet Ramatri amesema upasuaji umekuwa na mafanikio baada ya kufanyiwa upasuaji mara mbili; upasuaji wa kwanza ulikua wa kutoa kwanza meno manne na baadaye akatolewa meno matatu.

Wazazi wa mtoto huyo waligundua kuwa mtoto wao hanyonyi vizuri hivyo kuamua kumpeleka Hospitali ili kufanyiwa uchunguzi ndipo madaktari walipogundua mtoto huyo ana tatizo hilo ambapo hata hivyo daktari huyo ameeleza haijulikani kama upasuaji huo utaathiri uotaji wa meno wa mtoto huyo kwa siku za usoni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post