DEREVA WA TUNDU LISSU ASAKWA NA JESHI LA POLISI


Dereva wa Tundu Lissu akiwa ameshikilia nguo za Tundu baada ya kupigwa risasi.

Jeshi la polisi mkoani Dodoma limeagiza Dereva wa Tundu Lissu kujisalimisha Polisi haraka iwezekanavyo kwa ajili ya uchunguzi wa awali kuhusiana na tukio la mbunge wa Singida Mashariki,mwanasheria mkuu wa CHADEMA na rais wa TLS,Tundu Lissu kupigwa risasi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo,Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amemtaka dereva huyo ajisalimishe polisi.

"Polisi inamtaka dereva wa Tundu lissu ajitokeze na afike Polisi Dodoma bila kukosa au makao makuu ya upelelezi Dar es salaam ili aweze kutoa maelezo”,alisema Muroto

“Kutoweka kwake na kujificha ni kosa la jinai na kama kuna mtu au watu wanamficha wanatenda kosa la jinai, wamfikishe Polisi bila kukosa kwa kuwa ni shahidi muhimu katika upelelezi”,aliongeza Muroto.

Aidha asema magari 8 pia yamekamatwa aina ya Nissan na Watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa ili kubaini ni kina nani wamefanya shambulizi hilo kwa Tundu Lissu ambapo Jeshi la Polisi bado linaendelea kutoa wito kwa Wananchi wenye taarifa za tukio hilo waendelee kuzifikisha Polisi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post