Picha : JINSI SHABIKI ALIVYOTINGA UWANJANI NA KUMKUMBATIA ROONEY NA KUDAKWA NA POLISIJioni ya Julai 13,2017 katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam ulikuwa na mtanange wa kukata na shoka kati ya klabu kutokea nchini Uingereza "Everton" dhidi ya klabu kutokea nchini Kenya "Gor Mahia" mchezo ambao uliandaliwa maalumu na kampuni ya michezo ya bahati nasibu "Betting" ya SPORTPESA.

Katika mchezo huo ulikuwa umejaa ufundi na nidhamu ya soka kwa kila timu ulimalizika kwa klabu ya Everton kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Gor mahia.

Kilicho washangaza wapenzi wa soka ni pale ambapo shabiki mmoja alipovamia uwanjani na kumkumbatia Rooney na jeshi la polisi kufanya kazi yake kwa kumuondoa uwanjani pale.
Baadaye polisi walimuachia huru shabiki yule.

Baadhi ya picha kutoka uwanja wa Taifa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post