MSICHANA KUFUNGWA JELA MIAKA 10 KWA KUDANGANYA KUWA AMEBAKWA

Msichana mkazi wa Texas, Marekani ambaye alikimbilia Kanisani na kudai kuwa amebakwa na kundi la Wanaume watatu wenye asili ya Afrika, huenda akahukumiwa kifungo jela baada ya kukiri kwamba alidanganya.

Breana Harmon, mwenye umri wa miaka 19, mapema mwezi March alikimbilia Kanisani mjini Denison, Texas, akiwa na nusu uchi na mwili wake ukiwa damu na kudai kubakwa na wanaume wawili wakati mwingine akimshikilia chini, unaripoti mtandao wa KXII.

Hata hivyo, vipimo vya Hospitali havikuonesha ushahidi wowote kuwa msichana huyo alidhalilishwa na wanaume hao wenye asili ya Afrika ambapo wiki mbili baada ya tukio hilo alikiri kwa Polisi kuwa alidanganya juu ya tukio hilo na kuumia kwake kulitokana na yeye mwenyewe.

Kwa mujibu wa Mwanasheria Joe Brown, msichana huyo alifunguliwa kesi ya jinai mapema wiki hii kutokana na kudanganya ambapo thamani ya kosa ni kifungo cha hadi miaka 10 jela na faini ya Dollar 10,000.

“Tulivyoangalia katika kilichotokea kwenye kesi hii, na kuzingatia madhara iliyosababisha, na pengine itakayosababisha, tunaamini alichokifanya kinastahili adhabu zaidi. Alichokifanya ni kikubwa, na tunaamini ilikuwa ni kosa la jinai.” – Joe Brown.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post