DAKTARI ALIYEKUWA ANAWAONGEZEA WANAWAKE MAUMBILE YA KIKE AUAWA

Silikoni za vidole kama zinavyoonekana

Mwanamke mmoja nchini Brazil ambaye alikuwa akijihusisha na uwekaji wa vifaa vya kukuza maumbile ya kike kinyume cha sheria amekufa katika shambulio lenye viashiria vya ulipizaji kisasi baada ya upasuaji ambao haukuzaa matunda.

Marcilene Gama amekuwa katika lindi la mzigo wa lawama kutoka kwa wateja wake kutumia mchanganyiko wa madini ya silika kukuza makalio ya wateja wake wa jinsi ya kike.

Wakati akikaribia kifo chake, alikabiliwa na mkono wa sheria mahakamani kwa kosa la kujifanya daktari. Polisi mjini Rio de Jeneiro wanamsaka mwanamume aliyeonekana kwenye mkanda wa video wakati akiingia nyumbani kwa mwanamke huyo usiku wa jumamosi, kabla ya mwili wa mwanamke huyo kuonekana mtaa wa jirani.

Wachunguzi wanaoufanyia utafiti mwili huo wanaeleza kuwa mwili wa bi Gama, ulishuhudiwa huku mikono ya mwanamke huyo ikiwa imefungwa kwa nyuma, na kwamba uso wake ulionesha kuwa ulishambuliwa .

Ndugu wa bi Gama wameshangazwa na taarifa za kuwa ndugu yao alijiita daktari kwani wao wanadai kutokuwa na taarifa hizo, na mara zote wakati wa uhai wake alikuwa akiwaonya wateja wake juu ya matokeo ya upasuaji wa kuongezewa silika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post