CHADEMA WAZUIWA KUMUAGA MAREHEMU NDESAMBURO UWANJA WA MASHUJAA


June 3, 2017 kutoka Moshi Kilimanjaro ni kwamba wakati Maandalizi ya mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Moshi Mjini Philemon Ndesamburo yakiendelea, OCD Moshi amewaambia CHADEMA shughuli za kuuga mwili huo zitafanyika Majengo Uwanjani sio Mashujaa.

Mbunge wa Arusha mjini, Mh. Godbless Jonathan Lema amedai Vyombo vya usalama vimezuia kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Moshi mjini Mh. Philemon Ndesamburo kwenye uwanja wa Mashujaa. 

Hatua hiyo inakuja ikiwa tayari maandalizi yameanza kufanywa katika Uwanja wa Mashujaa kwa ajili ya kuuga mwili wa Ndesamburo lakini OCD Moshi amezuia na kusema shughuli hiyo itafanyika Majengo badala ya Mashujaa kuepuka kuzuia shughuli za kila siku.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post