ALIYEKUWA MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID MWAMBUNGU AMEFARIKI DUNIA

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu amefariki dunia leo saa nne asubuhi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)

Mdogo wa marehemu, Shaibu Mwambungu amesema kaka yake alifariki dunia leo asubuhi baada ya hali yake kubadilika ghafla akiwa hospitalini hapo.

Shaib amesema taratibu za mazishi zitatolewa baadaye ambapo kwa sasa anajiandaa kusafiri kutoka Songea kwenda jijini Dar es salam kwa ajili ya mazishi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post