EWURA YATANGAZA BEI MPYA YA MAFUTA YA PETROLI,DIZELI NA MAFUTA YA TAA..TAZAMA HAPA BEI ZOTE


Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza mabadiliko ya bei za mafuta nchini zitakazoanza kutumika kuanzia kesho, huku mafuta ya petroli yakionekana kushuka.

Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya petroli, dizeli na ya taa zimebadilika ikilinganishwa na bei za Machi Mosi mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo katika Makao Makuu ya ofisi za EWURA, Meneja Mawasiliano ma Uhusiano wa EWURA, Titus Kaguo amesema, bei ya reja reja ya petroli imepungua kwa Shilingi tatu kwa lita ambayo ni sawa na asilimia 0.13, pianbei ya jumla imepungua kwa Shilingi 5.65 kwa lita sawa na asilimia 0.29.

Aidha Kaguo amesema bei ya rejareja ya Dizeli imepanda kwa Shilingi saba kwa lita sawa na asilimia 0.36 wakati bei ya jumla ikiwa imepanda kwa Shilingi 3.68 kwa lita sawa asilimia 0.21.

"Hii shilingi tatu inaweza kuonekana ni ndogo lakini ina impact () kubwa sana kwa jamii, kwa kiasi kikubwa mabadiliko haya yametokana na mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia, mfumuko wa bei, pia gharama za usafirishaji ikilinganishwa na mwezi uliopita," amesema Kaguo.

==>Bei zote ziko hapo chini.....Tazama jedwali hili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post