KUHUSU AJALI YA BASI LA ABOOD NA HAPPY NATION, LORI KUGONGANA MLIMA KITONGA


Mabasi ya abiria ya Abood na Happy Nation kutoka Mbeya kwenda jijini Dar es salaam  yamepata ajali mlima Kitonga leo mchana. 

Taarifa kutoka kwa mashuhuda waliokuwa eneo la tukio wameeleza kuwa katika ajali hiyo wamejeruhiwa abiria 12. 

Mmoja wa Mashuhuda wa tukio hilo alieleza kuwa ajali hiyo imetokea baada ya basi la Abood kukosa breki na kuligonga roli la FM ambalo halikuanguka lakini liligonga Fuso iliyokuwa imebeba ndizi na kutumbukia korongoni baadae likaigonga basi la Happy Nation na mabasi yote kutumbukia korongoni . 

Taarifa rasmi kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto Mkoa wa Iringa Kamanda wa Jeshi la zimamoto mkoa wa Iringa Kenedy Komba akiwa eneo la tukio ametihibitisha kutokea kwa ajali hiyo, akielezea kuwa taarifa za awali majeruhi ni 12 na kati ya hao majeruhi watatu wamekimbizwa hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi, na kwamba hakuna vifo vilivyotokea katika ajali hiyo.

Moja ya Lori lililogongwa na kumbukia korongoni

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post