MAAMUZI YA MAHAKAMA KUHUSU WASANII WALIOPANDISHWA KIZIMBANI KWA DAWA ZA KULEVYA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imetoa maamuzi kwa baadhi ya wasanii waliokuwa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Mahakama hiyo imekubali maombi ya Jamhuri kuhusu tuhuma zinazomkabili Petitman na wenzake wanne kwamba watakuwa nje kwa dhamana ya shilingi milioni 20 na watatakiwa kuripoti kituo cha polisi mara mbili kwa mwezi kwa muda wa miaka mitatu na kila mmoja anatakiwa kuwa na mdhamini mmoja mwaminifu.

Aidha kwa TID, Tunda, Recho, Rommy Jones, Babu wa Kitaa na Nyandu Tozi watakuwa chini ya uangalizi kwa mwaka mmoja na dhamana ya Tsh milioni 10, wakivunja masharti watarudi Mahakamani

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post