MGONJWA ASHINDWA KUPATA HUDUMA MUHIMBILI KWA KUWA NA UREFU USIO WA KAWAIDA

Kijana Baraka Elias Mashauri mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa Musoma mkoani Mara ameshindwa kupata matibabu katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) kutokana na urefu wake usio wa kawaida.


Baraka anayesumbuliwa na tatizo ya nyonga ana kimo kirefu cha zaidi ya futi 7 na hii kufanya kushindwa kupatiwa matibabu kufuatia vifaa katika taasisi hiyo ikiwemo mashine za X- ray vitanda vya kufanyia upasuaji kuwa vifupi ukilinganisha na urefu wake.


Tatizo hilo la nyonga linalomsumbua Baraka limemfanya ashindwe kutembea na kulazimika kutumia magongo ambayo anasema yanamtesa kutokana na urefu alionao.


Akizingumzia jinsi watu wanavyomshangaa kutokana na urefu wake alisema kuwa kwake anaona fahari kwani ni maisha ambayo ameyazoea kila anapokwenda. Amesema kuwa hiyo haimpi shinda kwani anajua wanamshangaa kutokana na urefu wake kitu ambacho si kibaya.


Kuhusu ugonjwa unaomsumbua na baada ya kushindikana kupatiwa matibabu nchini, Baraka ameomba wasamaria wema waweze kumsaida ili apatiwe matibabu nje ya nchi ili arudie kwenye hali yake ya kawaida kwani magongo anayotumia kutembelea yanamtesa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post