Picha 31: UZINDUZI WA HUDUMA YA LONGA NA TAKUKURU SHINYANGA



Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Shinyanga leo imezindua huduma ya “Longa Nasi Kata Mnyororo wa Rushwa”,katika wilaya ya Shinyanga lengo likiwa ni kuwawezesha wananchi kutoa taarifa mbalimbali zinazohusu rushwa kwa kupiga simu ama kutuma ujumbe mfupi wa maneno (sms) bure TAKUKURU.


Huduma hiyo imezinduliwa leo Oktoba 15,2016 katika viwanja vya ofisi ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wilaya ya Shinyanga vilivyopo Nguzo Nane mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.

Huduma ya longa nasi kata mnyororo wa rushwa imeanzishwa na Taasisi ya Kupambana na Rushwa Tanzania TAKUKURU inawawezesha wananchi kupiga simu na kutoa taarifa za Rushwa kwa kupiga namba 113 au *113# yote ni kusaidia wananchi badala ya kwenda ofisi za Takukuru watakuwa wanatoa taarifa ambazo zitazingatia usiri.

Awali akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Gasto Mkono alisema lengo la kampeni hiyo ni kuamsha ari ya kupambana na rushwa itakayowazesha wananchi kutoa taarifa kwa njia ya simu.

“Huduma hii ya Longa Nasi ilizinduliwa kitaifa Mei 24,2016 na makamu wa rais Samia Suluhu Hassan, leo tumezindua rasmi katika wilaya ya Shinyanga”,alisema Mkono

“Huduma mpya ya 113 itasaidia wananchi kupiga simu ama kutuma ujumbe mfupi kwenda namba hiyo bure na kutoa taarifa au kuuliza maswali kuhusu rushwa , wananchi wanaweza kutumia huduma hiyo kwa wakati wowote na watahudumiwa moja kwa moja na maafisa wa TAKUKURU”,alieleza Mkono.

Alibainisha kuwa lengo la huduma hiyo ni kutoa wigo wa kutoa elimu sahihi ya mapambano ya rushwa na kwamba kupitia huduma hiyo watawafikia wananchi wengi katika maeneo yao.

Naye mgeni rasmi katika uzinduzi huo wa kampeni ya Longa Nasi mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alitumia fursa hiyo kuwataka watanzania wote kuungana pamoja kupiga vita rushwa kwani inakosesha watu haki zao na kurudisha nyuma maendeleo katika jamii.

“Mheshimiwa rais John Pombe Magufuli anachukizwa na vitendo vya rushwa,naombeni tumuunge mkono kwa kupiga vita rushwa kwa vitendo badala ya kulalamika na kuwaachia kazi TAKUKURU peke yao,tumieni huduma hii ya kupiga simu bure kuwafichua wanaopokea na kutoa rushwa”,alieleza Matiro.

Katika hatua nyingine aliwataka wananchi kutumia fursa hiyo kufichua vitendo vya uhujumu wa miradi inayoanzishwa katika jamii huku akiwaomba viongozi wa dini kutumia mafundisho ya dini kuwaelimisha wananchi juu ya madhara ya rushwa.

“Kampeni hii imelenga kuvunja ukimya, hivyo haitoshi tu kulalamika juu ya vitendo vya rushwa vinavyofanyika,inatakiwa kila mmoja wetu achukue hatua,viongozi wa dini,watendaji wa serikali na wananchi wote tuwe mstari wa mbele kupiga vita rushwa”,aliongeza Matiro.
Tazama Matukio katika picha yaliyojiri wakati wa uzinduzi wa huduma ya Longa Nasi Kata Mnyororo wa Rushwa-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Bango la TAKUKURU likiwa eneo la Viwanja vya Fire Nguzo Nane mjini Shinyanga.Bango linaoesha namba ya kulonga na TAKUKURU
Vijana wakiwa eneo la tukio

Kushoto ni mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga Gasto Mkono,kulia ni mgeni rasmi/Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro wakifuatilia burudani kwa njia ya nyimbo iliyokuwa inatolewa na vijana kutoka vikundi vya kupambana na rushwa katika shule za sekondari Uhuru,Samuye,Ngokolo la Klabu ya Tunaweza kutoka kata ya Ndala mjini Shinyanga
 Vijana kutoka kundi la Tunaweza Ndala wakiimba wimbo kuhusu rushwa na madhara yake katika jamii

Kushoto ni mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga Gasto Mkono,kulia ni mgeni rasmi/Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro wakiteta jambo
 Tunaweza wakiendelea kutoa burudani


Vijana wa klabu ya wapinga rushwa kutoka shule ya sekondari Samuye wakitoa burudani
Mchungaji Festo Mgasi akitoa neno wakati wa uzinduzi wa huduma ya Longa Nasi ambapo aliwataka watanzania kuepuka mkono wa rushwa kwani una madhara makubwa na kusisitiza kuwa viongozi wa dini wataendelea kukemea vitendo vya rushwa

Wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa kampeni hiyo


Sheikh wa mtaa wa Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga Majaliwa Masoud akitoa neno wakati wa uzinduzi wa huduma ya Longa nasi ambapo alisema rushwa ni haramu hivyo watanzania wamuunge mkono rais Magufuli katika vita dhidi ya rushwa

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga Gasto Mkono akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya Longa Nasi Kata Mnyororo wa Rushwa
Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga Gasto Mkono aliwahamasisha wananchi kutoa taarifa za rushwa kwa kupiga simu ama kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwenda namba 113 bure 
Tunfuatilia kinachoendelea hapa..

Mgeni rasmi/Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwahutubia wananchi waliohudhuria katika uzinduzi wa huduma ya Longa Nasi Kata Mnyororo wa Rushwa
Mkuu huyo wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alisema ni vyema sasa wananchi wakavunja ukimya kwa kufichua vitendo vya rushwa



Vijana wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Matiro alitumia fursa hiyo pia kuwahamasisha viongozi wa dini,watendaji wa serikali na wananchi kwa ujumla kukemea vitendo vya rushwa na kuepuka kulalamika tu na kuwaachia kazi TAKUKURU peke yao

Matiro aliwakumbusha pia TAKUKURU kufanyia kazi taarifa zinazotolewa na wananchi sambamba na kutunza siri za wananchi wanaotoa taarifa ili kuepuka kutowakatisha tamaa



Baada ya mgeni rasmi kuzindua rasmi huduma ya Longa Nasi Kata Mnyororo wa Rushwa-Kushoto ni mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga Gasto Mkono,akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro machapisho mbalimbali yatakayotumiwa na maafisa wa TAKUKURU katika kutoa elimu ya rushwa kwa wananchi

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa na washiriki mbalimbali wa uzinduzi wa makala ya sauti itayokuwa inatumika kutoa elimu ya rushwa katika maeneo mbalimbali

mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga Gasto Mkono,akiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(kushoto) eneo la tukio



Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga Gasto Mkono,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro,viongozi wa dini,vijana na wananchi wakiwa eneo la tukio


Viongozi wa dini,wanafunzi na wakuu wa idara katika wilaya ya Shinyanga wakiwa wameshikilia machapisho mbalimbali ya TAKUKURU


Picha ya pamoja viongozi wa dini na mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro

Picha ya pamoja wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Shinyanga na mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro



Picha ya pamoja wakuu wa idara katika wilaya ya Shinyanga na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro


Picha ya pamoja vijana kutoka kundi la wapinga rushwa wasio wanafunzi "Tunaweza"  na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro



Picha ya pamoja wanafunzi wa shule ya sekondari  Samuye na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro



Picha ya pamoja wanafunzi wa shule ya sekondari Uhuru na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro


Picha ya pamoja wanafunzi wa shule ya sekondari Ngokolo na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro


Picha ya pamoja baadhi ya wananchi na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527