BASI LA LAUA WATU 10, LAJERUHI 44 LINDI


 
Watu 10 wamefariki dunia na wengine 44 kujeruhiwa baada ya basi la Barcelona lililokuwa linatoka jijini Dar es salaam kwenda Mtwara asubuhi kuanguka katika eneo la Miteja mkoani Lindi.

Kamanda wa polisi mkoani Lindi Renatha Mzinga amesema ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Oktoba 17,2016 asubuhi.

Amesema waliopoteza maisha ni wanawake sita,mwanamme mmoja na watoto watatu na kwamba majeruhi ni wanawake 16 na wanaume 18,watoto watatu wa kike na saba wa kiume.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni tairi la mbele la basi hilo na kusababisha dereva apoteze mwelekeo.

Hata hivyo kamanda Mzinga amesema wanafanya uchunguzi zaidi juu ya ajali hiyo kwani basi hilo lilikuwa na abiria kupita kiasi na dereva amekimbia baada ya kutokea kwa ajali hiyo.

Amesema uwezo wa basi hilo ni kubeba abiria 48 lakini lilikuwa limebeba abiria 54 kinyume cha sheria za usalama barabarani.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post