Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
(NACTE) linapenda kuwaarifu wote walioomba kudahiliwa katika kozi mbali
mbali za cheti na diploma na Umma kwa ujumla kuwa uhakiki wa uteuzi wa
awamu ya pili kwa waombaji wa cheti na diploma umekamilika na kwamba
uteuzi huu sasa unaonekana kwenye kurasa binafsi (profile) za waombaji.
Hii ina maana kuwa waliochaguliwa sasa wanaweza kuona mahali
walipochaguliwa kupitia kurasa zao binafsi.
Hata hivyo, Baraza linaomba radhi kwa
kuwa uhakiki wa uteuzi kwa baadhi ya vyuo haujakamilika hivyo Baraza
litashindwa kuwaonyesha waombaji wa vyuo hivyo uteuzi wao. Vyuo hivyo ni
pamoja na vyuo vya kilimo na uvuvi na baadhi ya vyuo vikuu.
Baraza pia linapenda kuwaarifu
waombaji waliofanya maombi kwenye vyuo vya Ualimu vya Serikali kuwa
uteuzi kwenye vyuo hivyo bado unasubiri mwongozo wa Serikali na hivyo
watafahamishwa mara Baraza litakapopata mwongozo kutoka Wizara yenye
dhamana ya Elimu juu ya uchaguzi huo.
Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
NACTE
Tarehe: 10 Septemba, 2016
Social Plugin