Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

FUNDI UJENZI AKAMATWA NA BUNDUKI AINA YA SMG NA RISASI 69 MOROGORO



 NB-Siyo bunduki iliyokamatwa
****
FUNDI ujenzi Godfrey Fumbo (44) ambaye ni mkazi wa Mkundi katika Manispaa ya Morogoro, anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kukutwa na silaha moja aina ya Sub Machine Gun (SMG) na magazini moja pamoja na risasi 69 zikiwa zimehifadhiwa kwenye mfuko wa plastiki.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema mtuhumiwa alikamatwa juzi saa tatu usiku mlima Mzembe katika Kata ya Mkundi.


Kamanda Matei alisema mtuhumiwa hiyo alikamatwa na bunduki hiyo ya SMG yenye namba 56-1430284 pamoja na magazini moja yenye risasi 30 huku risasi nyingine 39 zikiwa zimehifadhiwa katika mfuko la plastiki zikiwemo risasi mbili za bunduki aina ya Rifle 375.



Kwa mujibu wa Kamanda Matei, kukamatwa kwa silaha hiyo ya kivita inayotumiwa na majeshi mbalimbali ilitokana na taarifa za kiintelijensia, zilizotumiwa na Polisi na kumkamata mtuhumiwa huyo.


Matei alisema baada ya kukamatwa na kumfanyia upekuzi nyumbani kwake, walipata magazini hizo na kwenda kuonesha mahali alipoficha silaha hiyo, ambayo ilikutwa ikiwa imefukiwa ardhini huku ikiwa imezungushiwa mkeka.


Alisema mtuhumiwa anahojiwa na hatua za kumfikisha mahakamani zinafuta, huku akiwashukuru wale wote waliotoa ushirikiano hadi kukamatwa kwa silaha na mtuhumiwa huyo na kuwataka kuendelea kutoa ushirikiano zaidi katika kupambana na uhalifu.

Via>>Habarileo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com