Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Breaking News!! TETEMEKO KUBWA LA ARDHI LAUA WATU ZAIDI YA 10 KAGERA-TANZANIA ANGALIA PICHA


image.jpeg 
Habari tulizozipata kutoka manispaa ya Bukoba mkoani Kagera zinasema kuwa kuna tetememko la ardhi limetokea na kusababisha madhara makubwa.


Tetemeko hili kubwa la ardhi linadaiwa kuwa na ukubwa wa Ritcha 5.7 limeikumbuka mikoa ya Kanda ya Ziwa hasa Kagera na Mwanza na kusababisha maafa makubwa ikiwemo nyumba za watu kubomolewa.

Maeneo yalioathirika zaidi kwa Tanzania ni, Bukoba, wilaya zote za Kagera na baadhi ya maeneo ya Mwanza. Aidha baadhi ya majeruhi ambao hawakuumia sana walitibiwa na kuruhusiwa kuondoka hospitalini hapo kurejea majumbani kwao.

Mbali na Mikoa hiyo ya Tanzania, pia tetemeko hilo limeikumba baadhi ya miji na majiji ya nchini Uganda ikiwemo KampalaMbarara iliyopo Kusini Mashariki mwa nchi hiyo.



Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mjini Bukoba, imeeleza kuwa watu 10 wamepoteza maisha kuokana na tetemeko hilo huku wengine zaidi ya 100 wakijeruhiwa vibaya na mpaka sasa wanaendelea kutibiwa hospitalini hapo.
ANGALIA PICHA NA SOMA HABARI KAMILI <<HAPA>>
Tazama picha nyumba zikiwa zimebomoka huko Bukoba

















 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com