WAZIRI WA HABARI AVIFUNGIA VITUO VYA RADIO 5 NA MAGIC FM KWA UCHOCHEZI

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametangaza kuvifungia kwa muda usiojulikana vituo vya Radio 5 ya Arusha na Magic FM ya Dar es Salaam kwa sababu za uchochezi.


Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Waziri Nape amesema kuwa vituo hivyo kwa nyakati tofauti vilitangaza habari ambazo ndani yake zina uchochezi.


“Adhabu hii ya kuvifungia kwa muda vituo hivyo viwili inaanza leo (Agosti 29 2016) hadi pale kamati itakapomaliza kazi yake,” alisema Nape.


Aidha, amesema kuwa ameiagiza kamati ya maudhui ya vyombo vya habari kuviita vyombo hivyo na kuvihoji kwa kina kisha kumshauri hatua zaidi ya kuchukua.


Waziri huyo ameeleza kuwa serikali inaendelea kutambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari katika kuleta amani na ushirikiano nchini na sio vinginevyo.


Hivi karibuni, Nape alitahadharisha kuwa vyombo vya habari vitakavyoripoti taarifa ambazo ni za uchochezi vitakumbwa na rungu la kuhusika kwa uchochezi pia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527