Kijana Auawa Kwa Kushambuliwa na Wananchi Baada ya Kuiba Kifaranga Cha Kuku Huko Mara



 
Mkazi wa Kijiji cha Nyisense wilayani Serengeti Mkoa wa Mara, Matiko Nyamanche (28) ameuawa kwa kupigwa na wananchi kwa tuhuma za wizi wa kifaranga cha kuku chenye thamani ya shilingi 1500.
 
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhani Ng’azi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 12 mwaka huu majira ya saa nne usiku.

Kamanda Ng’azi alisema siku ya tukio kundi la wananchi walimshambulia Nyamanche kwa silaha za jadi baada ya kutuhumiwa kuiba kifaranga cha kuku na mifugo mali ya Machele Mtatiro.
 
Alisema mtuhumiwa huyo alifariki dunia wakati akipelekwa hospitali

Ng’azi aliongeza kuwa watu 15 wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za mauaji hayo. 
 
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Senta, Ryoba Tamanya alisema kabla ya kukutwa na umauti Nyamanche alikuwa anakunywa pombe na wenzake na wakati anarudi alipita kwa shemeji yake Makere Mtatiro na kuiba kifaranga hicho na kukimbia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post