Picha 60 ! Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ashiriki Futari ya Pamoja Iliyoandaliwa na Meya wa Manispaa ya Shinyanga


Hapa ni nyumbani kwa meya wa manispaa ya Shinyanga ambaye pia ni mwenyekiti wa wenyeviti wa majiji,manispaa na halmashauri zote za wilaya nchini Tanzania ( ALAT),pia diwani wa kata ya Shinyanga mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi ( CCM) mheshimiwa Gulam Hafeez Abubakari Mukadam.

Usiku wa Julai 03,2016 meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam amewaalika viongozi mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga,waumini wa dini ya kiislam na wasio waumini wa dini hiyo kushiriki katika Futari ya pamoja ikiwa ni utaratibu aliojiwekea kila mwaka kufuturisha watu wa aina mbalimbali katika mwezi mtukufu wa Radhamani.

Futari hiyo kwa namna ya pekee mwaka huu imehudhuriwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Taleck,mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro,wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa na wilaya ya Shinyanga,sheikh mkuu wa mkoa was Shinyanga sheikh Ismail Habibu Makusanya,waumini wa dini ya kiislam,viongozi wa vyama vya siasa na wakazi wa Shinyanga wasio waislamu na wale wasio kuwa na dini.

Akizungumza wakati wa kufuturu meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam alisema kila mwaka hualika watu mbalimbali kushiriki naye katika futari ya mwezi wa Ramadhani na amekuwa akifanya hivyo kwa muda wa miaka takribani 30 sasa hata kabla hajawa kiongozi.

Alitumia fursa hiyo kuwaasa watanzania kushikamana na kuwa wamoja ili kuleta maendeleo katika nchi huku akiwataka wananchi kuunga mkono juhudi zinazofanywa na rais John Pombe Magufuli ikiwa ni pamoja na kutekeleza mambo anayoyaagiza.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Taleck mbali na kutumia fursa hiyo kujitambulisha kwa washiriki wa haflay hiyo fupi ya kushiriki futari aliwataka wakazi wa Shinyanga kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya kimaendeleo ili mkoa uweze kupiga hatua.

“Kitendo nilichokiona hapa kinanipa picha kuwa mna ushirikiano,nina watu wanaoshirikiana ambao naamini mtanisaidia katika kutekeleza majukumu yangu…tusiposhirikiana sisi wenyewe hata juhudi zinazofanywa na rais wetu zitakuwa siyo lolote,naomba viongozi wa dini kutuombea kwa mungu tuwe na afya na busara ya kuongoza”,aliongeza mkuu huyo wa mkoa aliyekuwa ameongoza na mme wake Alhaji Kidali

Kwa upande wake sheikh mku wa mkoa wa Shinyanga sheikh Ismail Habibu Makusanya mbali na kumpongeza meya kwa futari hiyo ,aliwataka watanzania kudumisha amani ya nchi iliyopo kwa ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha kuwa nchi inabakia kuwa salama.

Katika hatua nyingine alisema baadhi ya viongozi wanamchukia rais Magufuli kwa sababu rais amenyooka katika matendo yake lakini wao hawajanyooka “wamepinda” ndiyo maana wanashindwa kuendana na kasi yake hivyo kuwataka kubadilika ili kuifanya Tanzania kuwa nchi ya asali na maziwa.

Malunde1 blog ilikuwepo eneo la tukio,tazama picha 60 za matukio yaliyojiri ....
Sheikh wa mtaa wa Majengo mjini Shinyanga Balilusa Hamis akikaribisha wageni mbalimbali waliofika nyumbani kwa meya katika hafla fupi ya kufuturu pamoja
Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akiwakaribisha viongozi mbalimbali waliojitokeza kujumuika naye kupata futari ya pamoja
Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam (aliyesimama kulia) akizungumza wakati wa futari hiyo ambapo aliwashukuru kwa kujitokeza kwa wingi huku shukrani za pekee akizipeleka kwa uongozi wa mkoa wa Shinyanga kwani ni mara ya kwanza kupata ugeni mkubwa kiasi kile
Meya huyo wa manispaa ya Shinyanga aliwaomba watanzania kuendelea kudumisha ushirikiano na mshikamano kwani wote ni wa mungu


Wa kwanza kushoto ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa akifuatiwa na sheikh mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ismail Habibu Makusanya wakiwa nyumbani kwa meya

Wa kwanza kulia ni mme wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga bwana Yahya Kidali,wa pili ni mme wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga wakiwa nyumbani kwa meya wa manispaa ya Shinyanga
Washiriki wa tukio hilo wakitakari baada ya kumaliza kula
Viongozi wa vyama vya siasa na serikali,waumini wa dini ya kiislamu na wananchi wakiwa nyumbani kwa meya
Meya anaendelea kuzungumza
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna( wa pili kutoka kushoto) naye alikuwepo
Katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniface Chambi (aliyevaa kofia) naye alikuwepo
Washiriki wakiwa eneo la tukio

Mwandishi wa habari la gazeti la Majira bwana Suleiman Abeid akila futari
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa akizungumza katika hafla hiyo fupi ambapo aliwaomba watanzania kuendelea kupendana na kushikamana na kwamba viongozi wa chama chake wako tayari kushirikiana na viongozi walioteuliwa na rais Magufuli.Kulia ni mtangazaji wa radio Faraja ya Shinyanga bwana Steve Kanyefu akirekodi sauti kwa ajili ya vipindi vyake
Washiriki wa hafla hiyo walikuwa wakasaza....
Hafla inaendelea
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa akimpongeza meya wa manispaa ya Shinyanga kwa kuandaa futari na kukusanya watu wa Shinyanga kushirikia naye
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika hafla hiyo ambapo alimpongeza meya wa manispaa ya Shinyanga kwa kuona umuhimu wa kuwakutanisha wakazi wa Shinyanga bila kujali kuwa ni waumini wa dini ya kiislam
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro aliwaomba wakazi wa Shinyanga kuendelea kumpa ushirikiano ili kumaliza changamoto mbalimbali katika wilaya ya Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimkaribisha mkuu wa mkoa wa Shinyanga katika hafla hiyo

Add caption

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Taleck akizungumza katika hafla hiyo ambapo mbali na kujitambulisha aliwaomba wakazi wa Shinyanga kushirikiana naye kwa dhati katika kuendeleza mkoa wa Shinyanga
Mkuu  huyo wa mkoa aliwaomba viongozi wa dini kuendelea kuwaombea viongozi wa nchi kwa kuongoza ni kazi ngumu inahitaji msaada mkubwa kutoka kwa mungu.Wa pili kutoka kulia ni mkuu wa kituo cha polisi Shinyanga Pili Misungwi
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Taleck alisema yuko tayari kushirikiana na wakazi wa Shinyanga kuhakikisha kuwa mkoa wa Shinyanga unapiga hatua kubwa kimaendeleo
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Taleck akiendelea kuzungumza
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga akizungumza katika hafla hiyo
Sheikh wa mtaa wa Majengo mjini Shinyanga Balilusa Hamis akizungumza katika hafla hiyo
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga na viongozi wengine wakiwa nyumbani kwa meya wa manispaa ya Shinyanga
Tuko nyumbani kwa meya....
Tunafuatilia kinachoendelea hapa....
Sheikh mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ismail Habibu Makusanya akitoa shukrani zake ambapo alimpongeza meya wa manispaa ya Shinyanga wa kuandaa futari hiyo na kwamba amekuwa akifanya hivyo kwa muda mrefu kila mwaka,hivyo kuwaomba watoto wake kuiga mfano wa baba yao ambaye amekuwa akionesha upendo kwa watu watu wote bila kubagua dini wala makabila yao
Sheikh Makusanya pia alihamashisha upendo miongoni mwa watanzania 
Wa kwanza kushoto ni katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga bwana Stephen Mwita Wang'anyi akiwa nyumbani kwa meya wa manispaa ya Shinyanga
Tunafuatilia kinachoendela hapa....
Waumini wa dini ya kiislamu wakiwa nyumbani kwa meya

Wa kwanza kushoto ni mtoto wa meya,Abui Gulam Hafeez Mukadam akichukua matukio kwa ajili ya kumbukumbu
Sheikh Makusanya akizungumza
Sheikh Makusanya akisisitiza jambo
Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam (kulia) akifurahia jambo
Tunafuatilia kinachoendelea hapa...
Nyumbani kwa meya
Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akitafakari jambo
Sheikh wa mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akiendelea kuzungumza
Sheikh Balilusa akifunga hafla hiyo fupi
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna (kushoto) akiwa na katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniface Chambi
Picha za kumbukumbu zikaendelea kupigwa
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna akiwa na mkurugenzi wa Malunde1 blog,bwana Kadama Malunde (kulia).
Picha za kumbukumbu waandishi wa habari
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa na mme wake (katikati),wa kwanza kulia ni mme wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa na mme wake (katikati),wa kwanza kulia ni mme wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga wakifurahia jambo.



Picha zote na Kadama Malunde,Chibura Makorongo na Abeid Suleiman-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post