Mtalii Afariki Akijipiga "SELFIE" Mlimani Eneo Lisiloruhusiwa...Alikatazwa na Walinzi AkapuuziaMtalii kutoka nchini Ujerumani amefariki dunia baada ya kuanguka akijipiga picha nchini Peru.

Oliver Park, 51, alianguka kwenye eneo la mabaki ya kale ya Machu Picchu katika milima ya Andes nchini Peru.

Park alipuuza tahadhari za kiusalama na onyo kutoka kwa walinzi na akaenda eneo lisiloruhusiwa watu kujipiga picha.

Taarifa zinasema alienda kujipiga picha eneo la mwamba Jumatano.

Alijaribu kuruka juu ndipo ajipiga picha akiwa hewani lakini akateleza na kutumbukia kwenye bonde.

Maafisa wa uokoaji waliupata mwili wake Alhamisi na kuupeleka kituo cha polisi kilichoko karibu.

Polisi wamesema mwili wake utapelekwa chumba cha kuhifadhia maiti katika mji wa Cusco.
 
 Watu milioni moja walizuru Machu Picha mwaka 2014 wakiwa peke yao
via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post