Haya Ndiyo Maamuzi ya Mwisho ya Mahakama Kuhusu Kesi ya Oscar Pistorious


Mwanariadha mlemavu wa miguu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius leo amehukumiwa kifungo cha miaka 6 jela kwa kosa la mauaji ya mpenzi wake Reeva Steenkamp. Mwanariadha huyo tayari ameshatumikia kifungo cha takribani miezi tisa jela katika kosa la awali wakati alipopatikana na hatia ya kuua bila kukusudia mwaka 2013.

Kwa sasa kifungo chake kimeongezeka baada ya upande wa serikali kushinda rufaa hiyo ambapo kosa lake lilibadilika na kuwa kosa la kuua kwa kukusudia.

Hata hivyo katika tukio la aina yake mwezi uliopita wakati wa kusikilizwa kwa shauri hilo kuhusu adhabu aliyopewa mwanariadha huyo alishauriwa na timu ya wanasheria wanaomtetea walimshauri kuvua miguu ya bandia na kutembea kwenye chumba cha mahakama bila miguu hiyo.

Hatua hiyo ya kuvua miguu ya bandia iliyomfanya ashindwe kusimama vizuri ilikuwa na lengo la kumshawishi jaji ili auone udhaifu wake na kuamua ama amhukumu kutumikia jela kwa muda wote huo au la.

Hata hivyo upande wa mashtaka ulitoa hoja na kusema ulemavu wa mwanariadha huyo si jambo la msingi. Ambapo waliikumbusha mahakama kwamba Oscar Pistorius alimfyatulia risasi mpenzi wake Reeva Steenkamp mara nne alipokuwa amejifungia maliwatoni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post