Picha: Basi la UDA Lagonga Treni Jijini Dar es salaam


Basi la UDA lenye namba za usajili T 696 CVP limegonga treni katika eneo la Kamata Jijini Dar es Salaam wakati Basi hilo likotokea stendi ya Gerezani Kariakoo kuelekea Mbagala na kuua mtu mmoja na wengine zaidi ya 45 kujeruhiwa.
Ajali hiyo imetokea usiku wa Julai 26,2016.
 
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Ernest Matiku amesema majeruhi wamepelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu.


Hata hivyo, hakuweza kumtaja jina mtu huyo aliyefariki dunia.

“Ni kweli ajali imetokea kuna kifo cha mtu mmoja na watu wengi wameumia sana ,” amesema Kaimu kamanda huyo.


Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Mohammed Mpinga amethitisha kutokea kwa ajali hiyona kusema kuwa bado chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana na kikosi chake kinaendelea na uchunguzi na taarifa kamili itatolewa hapo baadaye.


Kwa mujibu wa mashuhuda chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi la UDA kupita katika barabara yenye njia ya treni bila kutii ishara ya kusimama kwa magari iliyokuwa imetolewa na mfanyakazi wa reli ili kuiruhusu treni kupita.








BOFYA <<HAPA>> KUONA PICHA NYINGI ZAIDI ZA AJALI YA TRENI NA BASI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527