Askari Polisi Aliyemuua Mwandishi wa Habari Daudi Mwangosi Ahukumiwa Jela Kifungo Cha Miaka 15

 
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mwenye namba G .2573 Pacificius Cleophace Simon (27).Mahakama kuu Kanda ya Iringa imemuhukumu kifungo cha miaka 15 jela askari Pasificus Simon kwa kosa la kumuua bila kukusudia aliyekuwa mwandishi wa habari Daudi Mwangosi wa channel ten.

Mauaji ya mwandishi huyo wa habari aliyekuwa pia mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa yalitokea kwenye vurugu zilizotokea Septemba 2, mwaka 2012 katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi wakati polisi walipokuwa wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakifungua tawi la chama hicho katika kijiji hicho.

Akitoa hukumu hiyo jaji mkuu wa mahakama kuu Tanzania Kanda ya Iringa Paul Kiwelo Amesema mahakama hiyo mara baada ya kukamilisha mashaurino na upande wa utetezi na Jamhuri na kumtia hatiani askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mwenye namba G .2573 Pacificius Cleophace Simon (27) mahakama imetoa adhabu ya kifungo cha 15 kutokana na kosa la kuua bila kukusudia.

Kushoto ni Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mwenye namba G .2573 Pacificius Cleophace Simon (27)


Marehemu Daudi Mwangosi
SOMA HABARI HII ZAIDI <<HAPA>>

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527