Angalia Picha!! Rais Magufuli Akiwa Kwenye Baraza la Eid El Fitri leo Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Julai 06 2016 amehutubia Baraza la Eid el-Fitr kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lililofanyika kitaifa katika viwanja vya Karimejee Jijini Dar es salaam.
Katika hotuba yake amemupongeza Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ali kwa juhudi zake za kuwaunganisha waislamu wote na kupanua wigo wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kutoa huduma za kijamii na ameahidi kuwa serikali ya awamu ya tano itaunga mkono juhudi hizo.

Rais Magufuli na Sheikhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhadi Mussa Salum mara baada ya kuwasili.
Rais Magufuli na Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya Baraza la Eid Elfitri.

Rais Magufuli amesema kitendo cha kuwaunganisha waislamu wote katika Baraza la Eid el-Fitr kinafungua ukurasa mpya na ni moja ya hatua muhimu za kuimarisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa waislamu wa makundi mbalimbali pamoja na watanzania wengine waisio waislamu.

Aidha Rais Magufuli amezungumzia juhudi zinazofanywa na BAKWATA katika kuimarisha taasisi zake zinazotoa huduma za kijamii na kulinda mali zake akisema serikali itahakikisha mali zote za waislamu zinakuwa salama na kwamba wote waliodhulumu mali za waislamu watazirejesha.





Rais Magufuli na Mufti Mkuu Sheikh Aboubakar Zubeir.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post