Angalia Picha- Mapokezi ya Rais Paul Kagame wa Rwanda Katika Ziara Maalum Nchini Tanzania


Rais Paul Kagame Rwanda akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake baada ya kuwasili katika aradhi ya Tanzania, Jijini Dar es Salaam leo kwa ziara maalum ya kiserikali kufuatia mwaliko wa Rais wa Tanzania.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Rais wa Rwanda Paul Kagame akiwa na mkewe Jeannette Kagame wakipokea zawadi ya maua mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam.

Rais wa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakifurahia vikundi vya ngoma za asili vilivyokuwa vikiburudisha mara baada ya Rais wa Rwanda kuwasili.

Rais wa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakifurahia vikundi vya ngoma za asili vilivyokuwa vikiburudisha mara baada ya Rais wa Rwanda kuwasili.

Rais wa Rwanda Paul Kagame akiwa na mwenyeji wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo rasmi na Rais wa Rwanda Paul Kagame pamoja na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Rwanda Paul Kagame akizungumza na Wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais Dkt. Magufuli.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais wa Rwanda Paul Kagame.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post