Watu Watano Wafariki Dunia Katika Ajali la Basi la NBS,Wengine Wajeruhiwa Ajali ya Basi la Kisbo SafariWatu watano wamefariki dunia papo hapo na wengine 35 kujeruhiwa katika ajali ya basi la kampuni ya NBS lenye namba za usajili T909BXK lililo kuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Tabora kuanguka katika eneo la Tabu Hotel kata ya Chigela wilaya ya Gairo mkoani Morogoro. 

Mganga wa hospitali ya wilaya ya Gairo Mushi Mabula amethibitisha kupokea maiti tano na majeruhi 26 ambapo amesema watu saba hali zao sinzuri na watahamishiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.

Kwa upande wao mashuhuda wakiwemo majeruhi wa ajali hiyo wameeleza jinsi ajali hiyo ilivyotokea huku mashuhuda wakiwataka madereva kuzingatia sheria za barabarani ili kuepusha ajali zisizo za lazima.

Miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro huku majeruhi wakilazwa katika hospitali ya wilaya ya Gairo.

Habari zingine zinadai kuwa ajali nyingine ni ya basi la Kisbo T895CYL limepata ajali ya kuparuzana na trailer flatbed eneo la Magubike Kilosa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post