Wahamiaji Haramu 4792 Wakamatwa Tanzania, Kati Yao 1796 Wamefukuzwa Nchini

Idara ya Uhamiaji imekuwa ikiendesha Operesheni ondoa uhamiaji haramu tangu mwezi Desemba mwaka jana katika operesheni hiyo iliyoonyesha mafanikio ambapo takribani raia 4792 wa kigeni wamekamatwa kwa kukiuka sheria, kanuni na taratibu za uhamiaji katika kipindi cha January hadi Aprili mwaka huu.


Akizungumza mbele ya wanahabari Kaimu Kamishna wa Idara ya Uhamiaji Abass Irovya amesema operesheni hiyo imefanikiwa ambapo raia 1796 wamefukuzwa nchini kwa kukiuka sheria za uhamiaji.

“Wananchi walio wengi wamekuwa wakitoa ushirikiano kwa Idara yetu kutokana na uelewa wao kuongezeka kwa sababu tunayo programu ya kutoa elimu kwa umma na imeonyesha mafanikio makubwa”,amesema Irovya.

Irovya aliongeza kuwa waliohukumiwa kifungo ni raia 132 na 383 kesi zao zinaendelea kwenye mahakama katika Mikoa mbalimbali hapa nchini.

Raia 388 walilipa faini hali iliyochangia kuongeza mapato ya Serikali kutokana na kukiuka sheria na Kanuni za uhamiaji hapa nchini. Kwa upande mwingine kesi 509 zinaendelea katika mahakama mbalimbali hapa nchini na raia 294 waliachiwa huru kutokana na mahakama kutowatia hatiani.

Idara ya Uhamiaji ina Vituo takribani 60 katika mikoa mbalimbali hapa nchini baadhi vikiwa katika Mikoa ya Tanga, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Katavi, Kigoma, Simiyu ambapo Idara hiyo imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu athari za raia wa kigeni wanaoingia nchini bila kufuata sheria na taratibu za Uhamiaji.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post