Tundu Lissu Awekwa Rumande Baada ya Kukosa Dhamana


MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amewekwa rumande kwa kukosa dhamana, mara baada ya mahojiano na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kufuatia kauli yake aliyoitoa jana inayoelezwa kuwa si ya kiungwana.



Mbunge huyo amehojiwa kwa saa tatu kuhusiana na maneno mengine ambayo anadaiwa kuyaandika kupitia mitandao ya kijamii kuwa ni ya uchochezi. 



Akizungumza na waandishi wa habari katika Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam jana, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amekiri kuwa Lissu amewekwa rumande kwa kukosa dhamana na hataachiwa leo, hivyo atalala huko mpaka kesho.

==> Hii ndiyo kauli iliyomfanya alale rumande

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527