Wabunge Watatu wa UKAWA Wasimamishwa Kuhudhuria Vikao vya Bunge,Yumo Mbilinyi,Kubenea na Ole Millya


Mbunge wa Mbeya mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Mbilinyi amesimamishwa kuhudhuria na vikao 10 vya Bunge kuanzi leo kufuatia kitendo cha kuonyesha kidole cha kati bungeni.



Joseph Mbilinyi alitenda kosa hilo alipokuwa akitoka nje ya ukumbi wa Bunge baada ya kile alichoeleza kuwa kuna mbunge wa CCM aliyemtusi mama yake. Hata hivyo alipohojiwa kama anamfahamu mbunge huyo, Mbilinyi alisema kuwa hamfahamu. 




Hukumu hiyo imesomwa leo na Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Bunge kueleza kuwa kamati hiyo ilijiridhisha kuwa kitendo kilichofanywa na mbunge huyo kuwa ni kosa. 




Aidha wabunge wangine waliosimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge ni pamoja na Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo, James Ole Millya Mbunge wa Simanjiro kwa makosa yanayofanana ya kusema uongo bungeni. Wabunge hawa wamesimamishwa kuhudhuria vikao vitano kuanzia leo. 



Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameahirisha mkutano wa tatu wa Bunge lililokuwa na lengo la kujadili na kupitisha bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha 2016 2017.

 Kufuatia kuahirishwa huko, kuanzia kesho Julai Mosi, serikali itaanza kutekeleza miradi na mpango mingine iliyoanishwa katika bajeti hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527