Yanga Noma!! Waishushia Kipigo GD Esperanca ya Angola,Matokeo Haya Hapa


Mei 7 ,2016 klabu ya Dar es Salaam Young Africans ambao mashabiki wao tayari mtaani wanajitamba na kujiita Mabingwa watarajiwa wa Ligi Kuu, wameshuka uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuwakabili wapinazani wao GD Esperanca katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika.



Yanga ambao walipangwa na GD Esperanca baada ya kutolewa na Al Ahly ya Misri jumla ya goli 3-2 katika michuano ya klabu Bingwa barani Afrika, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya wapinzania wao kutokea Angola klabu ya GD Esperanca, lakini Yanga watalazimika kwenda Angola wiki mbili zijazo kucheza mchezo wa marudiano.



Kipindi cha kwanza kilikuwa kigumu kwa pande zote na kwenda mapumziko bila kufungana, lakini awali Eperanca walikuwa wanacheza mpira wa taratibu na kujitahidi kumiliki mpira ili kuituliza presha ya mchezo, hali ambayo ilifanya Yanga wabadilke na kufanikiwa kupata goli la kwanza dakika ya 71 kupitia kwa Simon Msuva, kuingia kwa Matheo Anthony kulizaa matunda baada ya dakika ya 90 kufunga goli la pili.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post