Serikali Inaendelea Kuhakiki Madeni ya Walimu


WAZIRI wa Fedha na Mipango Mhe. Dakta Philip Mpango, ameliambia Bunge mjini DODOMA, jana tarehe 30, Aprili, 2016, kwamba serikali inaendelea kuhakiki madeni ya walimu yaliyowasilishwa kwa ajili ya malipo baada ya kubaini kuwepo kwa udanganyifu kwenye baadhi ya madai hayo


Alisema kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2015/2016, serikali ilipokea madai yenye jumla ya shilingi Bilioni 29 na Milioni 800 na imelipa 20.125bn, huku madai mengine yakizuiwa baada ya kubainika hayakuwa halali.


Alitolea mfano wa mtumishi mmoja aliyewasilisha madai ya shilingi 600m badala ya shilingi laki 6, huku madai mengine yaliyolipwa miaka ya nyuma yakiwasilishwa kama madeni mapya


Dakta Mpango alisema kuwa serikali inathamini mchango wa walimu katika maendeleo ya sekta ya elimu nchini na kwamba itaendelea kulipa madai yao na watumishi wengine wa umma baada ya kuyachambua, kuyahakiki na kujiridhisha kuwa ni halali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post