Rais Amfukuza Kazi Waziri Baada ya Video Ikimuonesha Akipiga Punyeto Ofisini Kusambaa Mtandaoni


Rais Jamhuri wa Kidemokrasi ya Congo, Joseph Kabila amemtimua kazi Naibu Waziri wa Posta na Mawasiliano kutokana na kusambaa kwa video inayomuonesha akipiga punyeto ofisini


Kwa mujibu wa televisheni ya taifa, RTNC, Kabila amedai waziri huyo, Enock Ruberangabo Sebineza ameliabisha taifa.

Tangu Alhamis iliyopita hadi Ijumaa, video hiyo imekuwa ikisambaa mtandaoni ikimuonesha waziri huyo akijichua ofisini kwake. Nyuma yake inaonekana bendera ya nchi hiyo na picha ya Rais Kabila.

Wananchi wengi wamekasirishwa na video hiyo na kumtaka ajiuzulu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post