Cristiano Ronaldo Hatacheza Mchezo Dhidi ya England Juni 2 2016
Monday, May 30, 2016
Kocha wa timu ya taifa ya Ureno Fernando Santos leo Jumatatu ya Mei 30 2016, amenukuliwa na vyombo vya habari hususani dailymail akithibitisha kuwa katika mchezo wa kirafiki kati ya timu yake dhidi ya timu ya Uingereza utakaochezwa June 2 2016 katika uwanja wa Wembley Cristiano Ronaldo na Pepe hawatacheza.
Fernando Santos amesema hayo kutokana na nyota hao kuwa na uchovu, kwani toka wamalize mchezo wa fainali ya Klabu Bingwa Ulaya kati ya klabu yao ya Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid uliochezwa May 28 2016 Milan Italia, hawajapata muda wa kupumzika hivyo wanahitaji wiki moja ya kupumzika.
Ronaldo na Pepe
“Siwapumzishi kwa sababu ya kukwepa majeruhi ila ni kwa ajili ya kuwaweka fiti tu, nafikiri Cristiano Ronaldo atajiunga na timu Jumamosi akiwa na hali ya kujiamini, ni mchezaji bora wa dunia na yeye ni muhimu kwa timu”
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com
🚧🚦 Usiendeshe gari lako bila Mafunzo na Leseni halali_ 📲 Wasiliana nasi sasa: wa.me/255740273285 Unahitaji nini? 🚘 Unataka kujifunza udereva wa magari na kupata Cheti? 📄 Una cheti unataka kupata Leseni? 🔄 Unajua kuendesha lakini huna cheti wala leseni na unataka refresh upate cheti? 🛣️ Una nyaraka zote muhimu lakini unahitaji kujifua zaidi barabarani? ✅ Una Leseni bila cheti na unataka renew? 🌍 Tupo mikoa yote Tanzania hadi vijijini! 📞 Tupigie sasa: 0769 763 285
Social Plugin