Chura ya Snura Yazua Balaa!! Afungiwa Kujihusisha na Masuala ya Sanaa,TCRA Yatakiwa Kufuta Video ya Chura Mtandaoni


Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo leo imetangaza kumfungia Snura kujihusisha na masuala ya sanaa.



Pia imeufungia wimbo wake Chura pamoja na video yake kutochezwa kwenye redio na TV nchini.
 Taarifa hiyo imetolewa na wizara hiyo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wake wa mikutano wizarani hapo jijini Dar. 




Uamuzi wa kumfungia umekuja kutokana msanii huyo kutojisajili kwenye Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA. 



Akiongea na waandishi wa habari, Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa wizara hiyo, Zawadi Msalla, amewaonya watu kutousambaza wimbo huo kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo WhatsApp. 



Amedai kuwa wale watakaokiuka agizo hilo watashtakiwa kwa kutumia sheria ya makosa ya mtandao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post