Angalia Picha!! Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo Vya Habari Duniani Leo Nchini Tanzania
Mgeni rasmi Mhe.Robert Vicent Makaramba (wa tatu kushoto) akiwa pamoja na wageni waalikwa wengine katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2016 yaloyofanyika Kitaifa katika Hoteli ya Malaika Beach Resort Jijini Mwanza yakiwa na Kauli Mbiu ya "Kupata taarifa ni haki yako ya msingi, Idai"


Mgeni rasmi Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramba (kulia) akifungua Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2016 akizungumza kwa niaba ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.Mohamed Chande Othman.
Akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Kimataifa akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Nape Nhauye,amesema Mahakama Kuu nchini iko tayari kutoa ushirikiano baina ya pande zote mbili ili kufanikisha kuwepo kwa Uhuru wa Vyombo vya Habari.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Nape Nnauye akitoa salamu zake katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2016.Nape amesema Wizara yake inatoa fursa ya kupokea mapendekezo juu ya suala la Urushaji wa Matangazo ya bunge Live (moja kwa moja) pamoja na kuhakikisha Sheria kandamizi kwa Vyombo vya habari ikiwemo sheria ya Magazeti ya Mwaka 1977 zinaondolewa.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Simon Berege, akitoa salamu za ufunguzi zake katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2016 ambapo
amesema maadhimisho hayo yanafanyika huku wanahabari wakiwa wanapitia manyanyaso kutoka kwa vyombo vya dola, Wanasiasa na wakati mwingine kutoka kwa wananchi ambapo mwaka jana kuliripotiwa kesi 30 za manyanyaso kwa waandishi wa habari.


Ametoa rai kwa Serikali kufuta uamuzi wake wa kuzuia wananchi kupata habari, kwa kuzuia matangazo ya shughuli za bunge kuonyeshwa moja kwa moja (Live), huku akivisihi vyombo vya habari vya kijamii kurusha live vikao vya mabaraza katika halmashauri nchini ili kutoa fursa kwa wananchi kufuatilia bajeti za halmashauri zao.


Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania akitoa salamu za ufunguzi katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2016 yanayofanyika Kitaifa katika Hotel ya Malaika Beach Resort Jijini Mwanza.

Usia Nkhoma ambae ni Afisa Habari, Shirika la UN Information Centre nchini Tanzania akitoa salamu zake katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2016 yaliyofanyika Kitaifa katika Hotel ya Malaika Beach Resort Jijini Mwanza.

Zulmira Rodrigues ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa UN nchini Tanzania, akitoa salamu zake katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2016

Wanahabari na Wadau wa Habari wakiwa katika katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2016 yanayofanyika Kitaifa katika Hotel ya Malaika Beach Resort Jijini Mwanza.

Dominica Haule kutoka GEMSAT akitoa salamu zake katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2016.

Mgeni Rasmi, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramba (wa pili kulia) akizindua Chapisho la sera ya Jinsia kwa Vyombo vya Habari vya Kijamii nchini.

Mgeni Rasmi, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramba (wa pili kulia) akizindua Chapisho la sera ya Jinsia kwa Vyombo vya Habari vya Kijamii nchini.

Picha ya Pamoja-Picha zote kwa Hisani ya Binagi Media Group Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post