Rais Magufuli: Shinyanga Ina Watumishi Hewa 226






Idadi ya wafanyakazi hewa katika mkoa wa Shinyanga ambao awali ulidaiwa kutokuwa na wafanyakazi hao kabisa, imeongezeka na kufikia 226.

Hayo yamebainishwa leo na Rais John Magufuli katika uzinduzi wa Daraja la Kigamboni, ambapo alisisitiza kuwa serikali yake haitawafumbia macho viongozi ambao kwa namna moja au nyingine wataruhusu mianya ya ubadhirifu wa fedha katika maeneo yao.
 
"Mkoa wa Shinyanga kwa taarifa nilizonazo hadi sasa wameshapatikana wafanyakazi hewa 226 kutoka ‘zero’ hivyo ni lazima tuwajibike kwa watanzania wanyonge” ,amesema Rais Magufuli.

Wakati wa kuwasilisha ripoti ya Mikoa Serikalini aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela alisema mkoa wake hauna mtumishi hewa hata mmoja ,jambo lililosababisha rais Magufuli kuunda tume iliyobaini watumishi hewa 45 katika awamu ya kwanza.

Baada ya kubainika uwepo wa watumishi hao, Rais alitangaza kutengua uteuzi wa Mkuu huyo wa Mkoa kwa kutokuwa makini na taarifa anazopewa na wasaidizi wake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post