RAIS MAGUFULI APIGA SIMU CLOUDS TV NA KUTAJA MSHAHARA WAKE,HUU HAPA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli amempigia simu mtangazaji wa kipindi cha ‪Clouds360‬ cha ‪‎CloudsTv‬, Hudson Kamoga baada ya kusikia watu wanazungumzia kuhusu mshahara wa Rais. 




Rais amesema mshahara alioukuta na ambao analipwa ni milioni 9 na laki 5 (9,500,000) na wala sio milioni 30 kama wanavyodai wapinzani. Amelazimika kuyasema hayo wakati wa uchambuzi wa magazeti kupitia Clouds360. 



Ameahidi akirudi kutoka likizo yupo tayari kuonyesha nyaraka za malipo ya mshahara wake.


Gazeti la Nipashe toleo la leo lilikuwa na habari iliyowanukuu Tundu Lissu na Zitto Kabwe wakitaka Rais Magufuli ataje Mshahara wake na aweke wazi kama anakatwa kodi ili kuondoa sintofahamu iliyopo .


Hivi karibuni, Dk. Magufuli aliahidi kupunguza mishahara ya baadhi ya vigogo inayozidi shilingi milioni 15 ili mtumishi anayepata mshahara mkubwa zaidi usizidi kiasi hicho.

CHANZO-MPEKUZIHURU.COM

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527