Picha !! Rais Magufuli Apokea Hati Za Utambulisho Wa Mabalozi Kutoka Nchi Mbalimbali Ikulu


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa nchi ya Jamhuri ya Czech hapa nchini Pavel Rezac, tukio hilo lilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Ikulu jijini Dar es Salaam Balozi Mteule wa nchi ya Jamhuri ya Czech hapa nchini Pavel Rezac.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Mteule wa nchi ya Jamhuri ya Czech hapa nchini Pavel Rezac mara baada ya kukabidhi hati zake za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi mteule kutoka nchi ya Jamhuri ya Sudani Kusini Mariano Deng Ngor aliyefika Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha hati yake za utambulisho.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Mteule wa nchi ya Jamhuri ya Sudani Kusini Mariano Deng Ngor aliyefika Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha hati yake za utambulisho.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Brazil hapa nchini Carlos Alfonso Iglesias Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Mteule wa Brazil hapa nchini Carlos Alfonso Iglesias Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Mteule wa Tanzania nchini Kuwait Mahadhi Juma Maalim Ikulu jijini Dar es Salaam. Balozi Mahadhi alifika Ikulu kwa ajili ya kuagana na Mhe. Rais kwa ajili ya kwenda kuanza kazi yake hiyo rasmi nchini Kuwait.

Kaimu Mnikulu Ngusa Samike kulia akimkaribisha Balozi Mteule wa Brazil Carlos Alfonso Iglesias Ikulu jijini Dar es Salaam katikati ni Kaimu Mkuu wa Itifaki James Mbwana kutoka Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kikanda na Kimataifa.


PICHA NA IKULU

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post