Mwanamuziki Tunda Man Apata Ajali ya Gari Akiwa na Wenzake Watano,Kuna Taarifa za Kifo na Majeruhi

Kama ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii utakuwa umekutana na taarifa inayomhusisha Tunda Man kupata ajali akiwa Mkoani Iringa asubuhi ya Aprili 17,2016, Tumempata Tunda Man mwenyewe na amekubali kutuelezea.


Maelezo ya mwanzo ya Tunda Man amesema

‘Tulikuwa tunatoka Njombe baada ya kumaliza show yetu na tukasema bora tusilale tuwahi kufika Dar,tumetoka Njombe saa 10 alfajiri mimi nikawa nasikia usingizi nikamwambia mwanangu hebu tuendeshe kidogo,kufika kijiji cha Idetelo kilomita kama 20 au 30 kabla ya kufika Mafinga tukiwa tumelala tukashtuka Gari inaingia porini tukasikia mshindo mkubwa gari imepiga puuuh Dereva hapo hapo akawa amefariki"
 
Tunda Man anamalizia kwa kusema

"Tulikua watu watano kwenye gari aliyekaa mbele na Dereva amevunjika mkono na nyama zimechanika,kuna mtu aliyekua nyuma mapafu yamepasuka,Mimi nipo poa,kwa sasa hivi tuko Mafinga hapa Hospitali ya Wilaya tunaangalia taratibu za kuchukua mwili tuupeleke Kilosa kwa ndugu zake,marehemu aliyefariki anaitwa Mussa lakini watu wengi wanamjua kwa jina la Man Katuzo"

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post