Kuhusu Ajali ya Ndege ya Shirika la Ndege la Auric Air Huko Bukoba


Abiria nane na marubani wawili waliokuwa kwenye ndege ya kampuni ya AURIC iliyokuwa ikitokea jijini Mwanza wamenusurika kifo baada ya ndege hiyo kupasuka tairi la mbele na kupoteza mwelekeo wakati ikijaribu kutua kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba.



Akizungumzia tukio hilo meneja wa uwanja wa ndege wa Bukoba, Doris Uagile amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya asubuhi na kwamba ndege hiyo ilipopasuka tairi ilikosa mwelekeo na kuelekea kwenye majani yaliyoko pembeni mwa uwanja huo.
 
Amesema katika tukio hilo kwamba hakuna mtu aliyejeruhiwa na abiria waliokuwa wasafiri na ndege hiyo kutokea Bukoba kuelekea Mwanza walitafutiwa usafiri mwingine.
 
Nao baadhi ya wananchi katika manispaa ya Bukoba walioshuhudia tukio hilo wamesema walisikia kishindo kikubwa na baadae wakaona ndege ikiingia kwenye majani.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527