Hot News!! Majambazi Watatu Wauawa Huko Kahama baada ya Kuvamia Duka na Kuua Watu Wawili


Jeshi la Polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga limefanikiwa kuuwa Majambazi watatu yaliokuwa yamevami duka la mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Emmanuel Mukumbo na kumuua kwa risasi ambapo majambazi hayo yalianza kujibizana risasi na Polisi baada ya raia wema kuijulisha polisi na kufika katika eneo la tukio.


Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kahama Bw.Vita Kawawa, amesema katika tukio hilo raia mwingine mmoja alipigwa risasi na majambazi hao na kupoteza maisha wakati akipelekwa hospitali huku akilipongeza jeshi la polisi kwa kazi nzuri waliyoifanya.


Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP Dismas Kisusi amewataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa jeshi la polisi punde wanapoona dalili zozote za kiuhalifu zinafanyika.


Katika tukio hilo jeshi polisi limefanikiwa kukamata bunduki mbili moja aina ya Short Gun na moja ya kivita aina ya Uzgun, bomu la kutupa kwa mkono, kisu cha kijeshi,risasi sitini,mkandawa kijeshi na magazine mbili za bunduki.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post