Baada ya Kumtumbua Jipu Anne Kilango,Magufuli Awageukia Mawaziri,Ametoa Kauli Hii


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Magufuli amesema amewatuma watu kuwarekodi mawaziri ambao wamesikika wakilalamika 'chinichini' kukatwa kwa fedha za matumizi mengineyo ( OC- Other Charges ) katika bajeti ya serikali ya mwaka ujao wa fedha.


"Mawaziri wengine nasikia wanalalamika kweli,sasa nimetuma watu kuwarekodi kwa sababu mind set (fikra) zao bado hazijabadilika,wanafikiri watu bado tupo kwenye trend hiyo hiyo,wasomi ni wengi,unaweza ukawateua leo na kesho ukawabadilisha, ili mradi twende kwenye trend ninayoitaka," alisema Magufuli.


Rais Magufuli aliyasema hayo jana Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia hatua ya bunge kubana matumizi na kuwezesha kupatikana kwa kiasi cha shilingi bilioni 6 ambazo zitaelekezwa kwenye utengenezaji wa madawati.

“Chief Secretary(Katibu Mkuu Kiongozi ), huo ndio muelekeo kwa Makatibu Wakuu, waache kudai OC… Nawasikia watu wanadai eti OC ni kidogo. Wakiona hazitoshi basi waache kazi, maana wenzao wabunge wamesema ni nyingi na wamebana matumizi," alisema Rais Magufuli na kuongeza:


"Katibu wa bunge ameonyesha mfano,kwa nini wengine washindwe? Mtaona katika bajeti tumekata hizo OC ambazo zilikuwa ni ulaji mtupu, tumeongeza bajeti ya maendeleo kutoka kati ya bilioni 26 na 27 hivi za mwaka jana hadi asilimia 40, fedha za bajeti ziende kufanya miradi ya maendeleo, zikawasaidie watu masikini."

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post