Angalia Picha!! Akina Mama Watoa Msaada wa Sare za Shule Kwa Watoto Waishio Katika Mazingira Magumu Huko Kishapu


Hapa ni katika shule ya msingi Maganzo iliyopo wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ambapo Aprili 27,2016 kikundi cha akina mama
kinachojulikana kwa jina la Liberation Group,ambacho sasa kina wanachama 15,kinachojihusisha na kusaidiana kwa akina mama hao ikiwemo kuinuana kiuchumi na kujengeana fikra chanya kimetoa msaada wa sare za shule kwa watoto 24 wanaosoma katika mazingira magumu kutoka shule nne za wilaya hiyo,Anaripoti Mwandishi wetu Marco Maduhu.


Shule zilizopata msaada huo ni shule ya Msingi Maganzo, Ikobabuki, Masagala na Ikonongo.Kikundi hicho kikiongoziwa na kaimu mwenyekiti wao Leocadia Masele wametoa sare hizo kwa watoto sita kila shule wanaoishi katika mazingira magumu. 
 

Watoto hao wanaishi katika mazingira Magumu wamepokea msaada wa sare za Shule kwa ajili ya kuondokana na adha ambayo wamekuwa wakiipata ya kusoma wakiwa na nguo chakavu na zilizochanika.Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo,kaimu mwenyekiti wa Kikundi hicho Leokadia Masele,mbele ya wanafunzi,walimu na viongozi wa serikali ya kijiji cha Maganzo,alisema kikundi chao kimekuwa kikisaidiana akinamama kuinuana kiuchumi na kujengeana fikra lakini baada ya kuona watoto hao wakisoma huku nguo zao zikikatisha tamaa ndipo walipoamua kutoa msaada huo wa sare za shule kwao.“Hakika uchungu wa mwana ajuaye mzazi hasa mwanamke, kauli hii imetugusa na kuona siyo vyema wanafunzi hawa wakaendelea kusoma katika mazingira magumu wakati sisi tuna uwezo wa kuchangishana na kuwapatia sare watoto hawa 24 jambo ambalo tuna amini watakuwa na furaha kwenye masomo yao,” alisema Masele.Masele alisema ni wajibu wa kila mmoja katika jamii kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu badala ya kuiachia serikali pekee. 
 

Mwenyekiti wa Kijiji cha Maganzo Sadiki Kangero, alikipongeza kikundi hicho cha akina mama hao kwa msaada walioutoa na kueleza kuwa ilifikia hatua baadhi ya watoto hao kuwa watoro shuleni.
 

Nao baadhi ya watoto hao walikiri kukata tamaa ya kuendelea na masomo kwa sababu ya mavazi yao kutia aibu kwa wanafunzi wenzao ,na kujiona kama wapo watupu (uchi) kutokana na nguo zao kuchanika na kuiona shule kama siyo sehemu salama kwao ya kutafutia ufunguo wa maisha.
 
Mwandishi wa Malunde1 blog,Marco Maduhu alikuwepo eneo la tukio ametusogezea picha yaliyojiri wakati wa zoezi la kukabidhi sare hizo za shule..Tazama hapa chini


Katikati ni kaimu mwenyekiti wa kikundi cha Liberation, Leocadia Masele na kaimu mwenyekiti wa kijiji cha Maganzo Sadiki Kangero(kulia) wakikabidhi sare za shule kwa wanafunzi hao wanaosoma katika mazingira magumu


Pokea zawadi ya sare ukasome kwa bidii


Wanafunzi wakiendelea kupokea msaada wa sare za shule

Wanakikundi cha Liberation wakikabidhi sare kwa wanafunzi hao

Zoezi la kukabidhi sare linaendelea

Mwanafunzi akipokea sare za shule


Mwanafunzi akipokea sare za shule


Pokea zawadi ya sare....

Zoezi la kukabidhi sare linaendelea

Zoezi la kukabidhi sare za shule linaendelea


Ninapokea sare mpya za shule....

Tunakabidhi sare za shule.....

Wanafunzi wakavaa sare mpya za shule walizopewa na kikundi hicho cha wanawake na kupiga picha ya pamoja

Tumependeza.....

Wanafunzi wakiwa wamevaa sare mpya

Wanakikundi cha Liberation wakiwa katika picha ya pamoja na walimu wa shule hizo na viongozi wa serikali ya kijiji cha Maganzo wilayani Kishapu

Picha ya pamoja-Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post