Picha 25!! Wadau Wa Usalama Barabarani Shinyanga Wakutana,Waunda Jukwaa La Kupambana na AjaliWajumbe wa Jukwaa la Usalama Barabarani manispaa ya Shinyanga wakiwa katika kituo kuu cha Polisi mkoa wa Shinyanga jana Aprili 27,2016 kushuhudia pikipiki 30 zilizokamatwa katika wilaya ya Shinyanga kutokana na madereva/waendesha pikipiki hizo kukiuka sheria za usalama barabarani ndani ya siku mbili Aprili 25 na 26 mwaka huu.
 
 
Jukwaa hilo la wadau wa usalama barabarani liliundwa jana wakati wa kikao cha wadau wa usalama barabarani walipokutana kujadili namna ya kukabiliana na ongezeko la ajali za barabarani mkoani Shinyanga.
 
 
Kikao hicho kiliandaliwa na kamati ya usalama barabarani mkoa wa Shinyanga kikiongozwa na mwenyekiti wa kamati hiyo Wilson Majiji na katibu wa kamati hiyo ambaye ni kaimu mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Shinyanga ACP Vicent Msami,ambaye ni mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Shinyanga. 


Kikao hicho kilikutanisha viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali,vyama vya siasa,taasisi za umma,mashirika,waandishi wa habari,waendesha bodaboda na makundi mengine mengi.

Wadau hao wa usalama barabarani katika manispaa ya Shinyanga walikubaliana kuunda jukwaa la wadau wa usalama barabarani kukabiliana na ongezeko la ajali za barabarani zinazogharimu maisha ya watanzania wengi kila kukicha.

Akizungumza wakati wa kikao hicho mwenyekiti wa jukwaa hilo Wilson Majiji ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani katika manispaa ya Shinyanga alisema jukwaa hilo litakuwa mstari wa mbele katika kupiga vita ajali zinazotokea barabarani.

Majiji alisema kutokana na ongezeko la ajali nchini hasa zinazotokana na pikipiki alisema ni vyema wadau wote wakaungana kufichua visababishi vyote vya ajali ili kuliepusha taifa kupoteza nguvu kazi.

“Jukwaa hili litapiga kelele pale panapokuwa na uvunjifu wa sheria za barabarani,hakuna alama za barabarani,tutatoa taarifa mahali panapohusika kama kuna hatari ya kutokea kwa ajali, na nguvu kubwa tutailekeza kwa waendesha bodaboda kwani ndiyo wanaongoza kwa kupata ajali”,alieleza Majiji.

Katika hatua nyingine wadau hao wa usalama barabarani walikubaliana kuwalipisha faini waendesha bodaboda waliokamatwa kwa kukiuka sheria za usalama barabarani,angalia picha hapo chini.

Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo wakati wa kikao hicho mpaka mwisho,ametuletea picha 25 angalia hapa chini

Kaimu mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Shinyanga mrakibu msaidizi wa polisi Vicent Msami akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa usalama barabarani manispaa ya Shinyanga kilichofanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi mkoa mjini Shinyanga.Alisema ajali nyingi hivi sasa ni za bodaboda na kutokana ajali kuwa janga kubwa linalopoteza nguvu kazi ya taifa
aliwataka wadau wote kuungana pamoja badala ya kuliachia jukumu jeshi la polisi pekee kwani kila mmoja ana wajibu wa kupambana na ajali za barabarani

Wadau wa usalama barabarani wakiwa ukumbini

Kaimu mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Shinyanga ACP Vicent Msami akizungumza katika kikao hicho,kulia ni mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Shinyanga Wilson Majiji,kushoto ni Afisa Mfawidhi SUMATRA mkoa wa Shinyanga Bahati Musiba
Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Shinyanga Wilson Majiji akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema kutokana na ongezeko la ajali nchini hasa zinazotokana na pikipiki ni vyema wadau wote wakaungana kufichua visababishi vyote vya ajali ili kuliepusha taifa kupoteza nguvu kazi.

Wadau wa usalama barabarani wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini


Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Shinyanga Wilson Majiji akizungumza katika kikao hicho


Askofu wa Kanisa la African Inland Church (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Dkt John Nkola akichangia mada katika kikao hicho ambapo alilipongeza jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kupitia kamati ya usalama barabarani kuona umuhimu wa kuwakutanisha pamoja wadau na kuunda chombo kitakachotumika kupiga vita ajali za barabarani.

Mjumbe wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Shinyanga Afridon Mkhomoi ambaye ni mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi Veta mkoa wa Shinyanga akizungumza katika kikao hicho ambapo aliwasihi watumiaji wa vyombo vya moto kupata elimu kuhusu sheria za usalama barabarani

Wadau wa usalama barabarani wakiwa ukumbini

Viongozi wa dini wakiwa ukumbini

Wadau wakiwa ukumbini

Wadau wa usalama barabarani wakiwa ukumbini

Tunafuatilia kinachoendelea

Wadau wa usalama barabarani wakiwa ukumbini

Tunafuatilia kinachoendelea ukumbini

Hapa ni katika kituo kikuu cha polisi mkoa wa Shinyanga,katikati ni kaimu mkuu wa kikosi cha usalama barabarani jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Mrakibu Msaidizi wa Polisi Vicent Msami akiwaonesha wajumbe wa Jukwaa la Wadau wa Usalama pikipiki 30 walizokamata ndani ya siku mbili kwa kukiuka sheria za barabarani ikiwemo wanaoendesha pikipiki bila leseni,kofia ngumu,wanaobeba watoto wadogo na wasio na leseni

Mwenyekiti wa Jukwaa la wadau wa usalama barabarani Wilson Majiji (wa pili kushoto) akizungumza kituoni hapo ambapo alisema jukwaa hilo kwa kushirikina na jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limewahurumia waendesha bodaboda waliokamatwa kulipa faini ya shilingi 30,000/=,badala ya kuwafikisha mahakamani baada ya hapo wakifanya makosa watapelekwa mahakamani
Mwenyekiti wa Jukwaa la wadau wa usalama barabarani Wilson Majiji akiwasisitiza waendesha pikipiki na wamiliki wa pikipiki kuzingatia sheria za usalama barabarani
Add captionWajumbe wa jukwaa la usalama barabarani wakiwa eneo la tukio

Pikipiki zilizokamatwa

Wajumbe wa jukwaa la usalama barabarani wakiwa eneo la tukio

Pikipiki zilizokamatwa

Kushoto ni baadhi ya wamiliki na waendesha pikipiki zilizokamatwa
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post