WABUNGE NA MAKADA WA CHADEMA WAFIKISHWA MAHAKAMANI




Wabunge wawili Mh.Halima Mdee wa Kawe na Mh.Mwita Waitara wa Ukonga wamepandishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na kosa la kumjeruhi mwili katibu tawala wa mkoa wa Dar es Salaaam Bi.Theresia Mbando katikia ukumbi wa Karimjee. 

Watumihiwa hao walipandiswa mbele ya hakimu mkazi Huruma Shaidi ambapo wakili wa serikali Mwamni Kombakono aliiambia mahakama kupitia hati ya mashtaka kuwa tarehe 27/02.2016 katika ukumbi wa Karimjee watuhumiwa hao wakiwa na wenzao wengine wawili akiwemo diwani wa kata ya Saranga walimjeruhi mama huyo.

Baada ya kusomwa kwa hati hiyo mahakama iliambiwa kuwa upelelezi haujakamilika ambapo jopo la mawakili wanaowatetea washtakiwa hao likiongozwa na wakili Peter Kibatala wakaiomba mahakama kuwapatia wateja wake dhamana ambapo Mh.Hakimu alikubali na kuwapa dhamana ya kujidhamini wenyewe kwa bondi ya shilingi milioni mbili kila mmoja.Kesi hiyo itatajwa tena March 16. 


Katika hatua nyingine mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya kupinga ubunge wa jimbo la Mafia baada ya mahakama hiyo kuona walalamikaji hao hawana sifa ya kulalamikia ushindi kwa sababu siyo wagombea ambapo mbunge wa Mafia Mh. Ramadhni Dau amesema haki imetendeka.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527