WALIOMPIGA DAKTARI HUKO MTWARA WAKAMATWA



Kufuatia tukio la ndugu wa mgonjwa kumpiga Daktari Mkoani Mtwara, tayari jeshi la Polisi Mkoani humo linawashikilia watu kadhaa kwa kitendo hicho cha kumpiga Daktari wakati akiwa katika majukumu yake ya kikazi.



Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara,Henry Mwaibambe (Pichani) amesema hadi sasa watu 2 wanaotuhumiwa kumpiga daktari hospitali ya Mkoa wamekamatwa usiku wa kuamkia jana wakitoroka nchini huku wengine 3 wakiendelea kusakwa.


Awali wauguzi na Madaktari wa Hospitali hiyo waligoma kufanya kazi hadi hapo watakapohakikishiwa usalama wao ndipo wafanye kazi


Jana, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu aliweza kufika Hospitalini hapo na kusuluhisha mgogoro huo huku akiomba Jeshi la Polisi kuongeza usalama kwa watumishi hao wa Afya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527