KUHUSU WACHIMBAJI WATANO WA MADINI KUFARIKI KWA KUFUNIKWA NA KIFUSI HUKO GEITA

Watu watano wamepoteza maisha na wengine watatu kujeruhiwa vibaya kwa kuvunjika viungo vyao baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakichimba mawe yanayodhaniwa kuwa ni dhahabu.

Tukio hilo limetokea jana saa 9:00 Alasiri, katika kata ya Mgusu Wilayani Geita ambapo watu hao waliangukiwa na ukuta wa udongo waliokuwa wakiuchimba.

Wakizunguza na channel Ten iliyofika katika kata hiyo baadhi ya wachimbaji waliokutwa katika eneo hilo wakaeleza hali ilivyokuwa.

Pamoja na tukio hilo la kusikitisha wachimbaji hao wakatoa kilio chao kwa Serikali kuhusu maeneo ya kuchimba yaliyo salama ikiwa ni pamoja na kuwapa zana za kuchimbia na uokoaji.

Katibu tawala ya wilaya ya Geita Gaspar Kanyaiita aliyetembelea eneo hilo ameagiza Ofisi ya Madini kuwakamata wachimbaji wote wanaokiuka kanuni huku kaimu Afisa Madini Mkoa wa Geita akisema eneo hilo limefungwa tangu jana mpaka itapotangazwa utaratibu mwingine.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527