JINSI MBUNGE ESTER BULAYA ALIVYOKAMATWA NA POLISI SAA SABA USIKU HUKO MWANZA


Mbunge wa jimbo la Bunda,Ester Bulaya amekamatwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza na kulazimika kulala rumande baada ya kunyimwa dhamana.


Polisi walivamia Hoteli aliyofikia mbunge huyo na kumkamata majira ya saa 7 usiku na kisha kumpeleka kituo cha kati cha Jijini Mwanza akiwa ameambatana na Mhe. Halima Mdee (Mb) , Joyce Sokombe (Mb) pamoja na Wakili John Malya.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Justus Kamugisha amesema hati ya kukamatwa kwake imetoka ofisi ya Bunge na kwamba Mbunge huyo anashikiliwa kama mtuhumiwa ambaye anatakiwa kusafirishwa kwenda Dar es Salaam.

Wabunge hawa pamoja na uongozi wa juu wa CHADEMA Wako jijini Mwanza kwa ajili ya kikao cha Baraza Kuu la chama hicho kinachofanyika leo katika Hotel ya Gold Crest

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527