RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE APATA UTEUZI MWINGINE MZITO




Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameteuliwa na Mheshimiwa Dkt. Nkosazana Dlamini Zuma, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (kulia) kuwa Mwakilishi wa Umoja wa Afrika katika mchakato wa usuluhishi wa mgogoro wa Libya.

Kufuatia uteuzi huo uliotangazwa rasmi na AU jana katika Kikao cha Wakuu wa Nchi za Afrika, Rais Mstaafu Kikwete leo asubuhi amekutana na Dkt. Zuma makao makuu ya AU leo na kufanya nae mazungumzo kuhusu jukumu alilokabidhiwa.

Mheshimiwa Dkt. Kikwete amemshukuru Dkt. Zuma na Wakuu wa Nchi za AU kwa imani kubwa waliyoonyesha kwake kwa kukabidhiwa jukumu hilo zito. Amewashukuru pia wadau wa siasa nchini Libya kwa kuridhia uteuzi wake.

Naye Dkt. Zuma amemshukuru Dkt. Kikwete kwa kukubali uteuzi huo na kuwa tayari kubeba jukumu hilo.


Amemueleza kuwa Umoja wa Afrika na Afrika nzima inayo matarajio makubwa juu yake na iko nyuma yake.


Amemuhakikishia kumpa kila aina ya ushirikiano atakaouhitaji kukamilisha katika kutekeleza majukumu yake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post